WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WAUNGA MKONO DAWA ZA CHANJO KWA WATOTO ZICHUNGUZWE KUTOKANA NA WATOTO KULEWA,KUANGUKA NA KUZIMIA WANAPOTUMIA DAWA HIZO-Agosti 2,2017
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi,wameunga mkono hoja ya baadhi ya madiwani waliotaka ziangaliwe upya dawa
za chanjo zinazosababisha wanafunzi wa shule za msingi kuanguka na kuzimia
baada ya kunywa dawa hizo.
Wakazi hao wakiwemo,John Pasua, Bi.Matengenezo
Rafiki wa Elia na mama Mariam,wamethibitisha kwa nyakati tofauti kushuhudia na
kusikia wanafunzi wakipatwa na tatizo la kuanguka mara baada ya matumizi ya
dawa hizo.
Hatua ya kutaka dawa ziangaliwe upya iliibuka jana
kupitia mkutano wa baraza la madiwani wa kufunga mwaka 2016 wa bajeti ambapo
imeonekana kuwa takribani wanafunzi 16 wameanguka na kuzimia baada ya kutumia
dawa hizo na hatimaye kufikishwa vituo vya huduma za afya.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya
Mpanda Michael Nzyungu kupitia mkutano huo amesema kuanguka kwa wanafunzi ni
matokeo ya maudhi madogomadogo yanayotokana na dawa hizo ambazo kimsingi hazina
madhara.
Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments