WAZIRI MKUU AELEZA AFURAHISHWA NA HALI YA CHAKULA MKOANI RUVUMA
Na.Issack Gerald.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati
ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.
Pia,
amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na
kufanyakazi, na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu mmoja
mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa mapokezi makubwa aliyopata.
“Nawapongeza
sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka kutoka shilingi 654,227,
hadi kufikia shilingi 1,800,000 kwa kipindi cha mika 4 tuendelee kujiweka
vizuri kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja” alisema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia amesisitiza kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yote
yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila kutegemea sana kipindi cha
masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu na kusisitiza matumizi
mazuri ya fedha zinazopatikana katika mazao hayo.
Kwa
upande wake, Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema zaidi ya asilimia 90 ya
wananchi wa Ruvuma hutegemea kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na
biashara yakiwemo mahindi, mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru na
Songea vijijini, korosho ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru, Namtumbo,
Nyasa, Mbinga na Songea vijijini na tumbaku maeneo ya Namtumbo,Mbinga
na Songea vijijini.
Alisema,
Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada kwa
kipindi cha mwaka 2012 - 2013, 2013 - 2014 hali hiyo imeendelea kuwa nzuri hadi
kipindi cha mwaka 2015 - 2016. Mahitaji yakiwa ni tani 469,172 na ziada ikiwa
tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za ongezeko hilo la tani ni
pamoja na matumizi ya dhana bora za kilimo, matumizi ya pembejeo za
kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo, aliongeza Mkuu wa Mkoa.
Waziri
Mkuu Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya kikazi
ya siku nne mkoani Ruvuma, kesho siku ya jumatatu atakuwa na
shughuli za kufungua tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua
maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya
Songea na kukagua Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Kupitia
ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa shughuli za
maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na kuweka msisitizo
katika maeneo yaliyopewa kipaumbele hasa katika sekta ya Afya.
Asante kwa kuendelea
kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
Chanzo
cha habari :Ofisi ya mawasiliano ya Waziri
Comments