WAWILI MPANDA WAUAWA,WAUAJI WATOKOMEA KUSIKOJULIKANA NAO POLISI WASEMA HAPA KAZI TU
Na.Issack Gerald-MPANDA
Watu
wawili wamekutwa wakiwa wameuawa na watu wasiojulikana Wilayani Mpanda Mkoani
Katavi baada ya kukatwa na vitu vyenye ncha kali Januari Mosi Mwaka huu.
Mratibu
wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi SSP Focas Malengo amesema,katika tukio la
kwanza mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Tiho Robert (40) mkazi wa kitongoji
cha Center John kijiji na kata ya Mwamkulu Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,aliauawa
majira ya saa tano za usiku.
Katika tukio hilo,marehemu alivamiwa na
wauaji hao akiwa amelala nyumbani kwake baada ya kuvunja mlango na kuanza
kumshambulia ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo walikimbia na kutokomea
kusikojulikana.
SSP
Malengo amesema,katika tukio lingine,mwanaume aliyekadiriwa kuwa na umri kati
ya miaka 25-30 aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na
shingoni na watu wasiofahamika ambapo alikutwa katika maeneo ya mtaa na kata ya
Nsemulwa amjira ya saa mbili asubuhi.
Hata
hivyo chanzo cha mauji ya watu ahawa hakijajulikana na Jeshi la Polisi limesema
Linaendelea na upelelezi ili kuwabaini wahusika na kuwafikisha katika vyombo
vya kisheria.
Asante kwa kuendelea kuwa namii,endelea
kuhabarika na P5 TANZANIA
Chanzo cha habari :Mratibu wa Jeshi la Polisi kny ya RPC
Katavi
Comments