NDEGE IMEANGUKA ARUSHA NA KUUA WATU 11



Shirika la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali ya ndege iliyotokea jana  asubuhi limesema watu wote 11 waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki dunia.
Coastal wameeleza kuwa,ndege yao Cessna Caravan ilipata ajali majira ya saa 5 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki katika eneo la Empakaai,Ngorongoro ikiwa na rubani mmoja na abiria 11 wakati ikiwa safarini kuelekea Serengeti.
Shirika hilo limesema majina ya waliofariki katika ajali hiyo bado hayajawekwa wazi wakisubiria kuwajulisha ndugu zao.
Mkurugenzi Mkuu wa Coastal,Julian Edmunds amesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana, na kwamba mara kadhaa amekuwa akisafiri na ndege za shirikia hilo na hivyo anaimani na marubani pamoja na ndege zao.
Aidha,ameeleza kuwa kwa niaba ya shirikia hilo na wafanyakazi wake, watafanya kila litakalowezekana ndani ya uwezo wao kusaidia katika uchunguzi wa ajali hiyo kwani hakuna kitu cha umuhimu kwao zaidi ya usalama wa abiria.
Kwa sasa wameeleza kwamba wanafanya uchunguzi katika eneo la tukio na kuwa, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo watazitoa mara taarifa kamili zitakapopatikana.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA