MKOA WA KATAVI KUPATIWA MADAKTARI BINGWA
Na.Issack Gerald
Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa miongoni
mwa mikoa itakayopatiwa madaktari bingwa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa
wangonjwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu
waziri wizara ya Afya Dk Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la nyongeza
lililoulizwa na Mbunge wa viti maalumu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo
CHADEMA Roda Kunchela aliyetaka kujua lini serikali italimaliza tatizo hilo.
Akijibu swali hilo amesema tayari serikali imeanza kuchukua hatua za haraka
kulikabili suala hilo kwa mkoa wa Katavi na maeneo mengine.
Licha ya hayo
serikali ya mkoa wa Katavi iko mbioni kuanza ujenzi wa hosipitali ya rufaaa
itakayo toa huduma kwa mkoa mzima ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 1
ilikwishapatikana kwa ajili kuanza ujenzi wa Hospitali hiyo.
Mwezi
Julai mwaka huu,Waziri wa afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia ,wazee na watoto
mh.Ummy Mwalimu aliahidi kuleta pesa mkoani Katavi ili kuongeza nguvu katika
ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Katavi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments