IGP SIRRO AWAHAKIKISHIA USALAMA WATANZANIA WOTE KIPINDI CHA PASAKA
Amesema
Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro matukio makubwa ya uhalifu wa
kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
IGP
Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ili kutoa
salaamu za pasaka kwa watanzania ambapo amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano
wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi jambo ambalo limesaidia kupunguza
uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
Aidha
amesema jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea
ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.
Katika
hatua nyingine amesema jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia
wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu
na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na vitakapojitokeza
vitadhibitiwa kwa haraka.
Ulinzi
utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia,fukwe,sehemu za
starehe na sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi
wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya utulivu.
Kwa
upande wa wazazi wametakiwa kuwaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke
yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu pia wamiliki wa kumbi za starehe
wanatakiwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo
ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.
Vilevile
Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara
kuwa makini na kuzingatia Sheria za Usalama barabarani hasa kwa madereva wa
magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi,kubeba mishikaki,kwenda
mwendo kasi,kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Habari kamili ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments