WANAFUNZI 15 WAMEHITIMU ELIMU YA BIBLIA

Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya biblia FPCT Katumba Wakiwa na baadhi ya watumishi Mpanda Radio
Viongozi wa dini Mkoani Katavi wameaswa kutumia taaluma na karama zao katika kuunganisha jamii inayomtambua mungu mionyoni mwao na kuhimiza waumnini kutotenda matukio yanayoleta athari kwa jamii hapa nchini.
Wito huo umetolewa jana na Mchungaji Zacharia Andrea kutoka chuo cha Biblia Bigabilo kilichopo mkoani Kigoma,aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa shule ya biblia FPCT Katumba yaliyofanyika Misheni ya Katumba akisema viongozi wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa matendo mema.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya biblia FPCT Katumba Mchungaji Elisha Musenda,katika taarifa yake amesema,shule ya biblia FPCT Katumba,imesaidia kupatikana viongozi wazuri wa kanisa wanaoshirikiana na jamii katika kuleta maendeleo hapa nchini.
Katika risala ya wanafunzi ambayo imesomwa na mwinjilisti  Moris Samson,wameomba mafunzo yawe endelevu katika shule hiyo huku Mchungaji kiongozi wa kanisa la FPCT Katumba Mchungaji Wilium Isaya  akisema kuendelea kwa mafunzo katika shule hiyo ni maamuzi ya kanisa ngazi ya taifa.
Jumla ya wanafunzi 15 wa shule ya biblia FPCT Katumba wamehitimu elimu ya mwaka mmoja wa ngazi ya cheti kwa mwaka 2017 na kufanya kuwa mahafali ya 13 tangu miaka ya 1990 yalipoanza kwa mara ya kwanza.

HABARI ZAIDI NI P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA