JAMII MKOANI KATAVI IMETAKIWA KUSHIRIKI KUWAFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU WALIOFICHWA MAJUMBANI ILI WAPATE HAKI YAO YA ELIMU
Na.Issack Gerald-Katavi
JAMII Mkoani Katavi imeaswa
kushirikiana ipasavyo na kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu iliyopo
Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kwa kuwafichua watoto waliofichwa majumbani ili
wapatiwe haki ya elimu.
Wanafunzi wenye ulemavu na wasio na ulemavui katika shule ya msingi Azimio Manispaa ya Mpanda wakiwa katika picha ya pamoja(PICHA NA.Issack Gerald) |
Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Mradi
wa elimu jumuishi Tanzania Alani Kamunde wa shirika la International Aid
Services,kupitia kikao cha kupokea,kujadili,kutathimini na kupanga mikakati ya namna
ya kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakbili watoto wenye ulemavu Mkoani
Katavi.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa
elimu Jumuishi mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronica Mavanza amesema,matatizo
yanayowakabili watoto wenye ulemavu yaliyobainishwa na kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wameyachukua na
watashirikisha jamii ipasavyo kuyapatia ufumbuzi.
Naye mwenyekiti wa kamati ya kulea
baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda Bw.Joshua Sankara ambaye pia
anatoka idara ya maendeleo Manispaa ya Mpanda,amewapongeza viongozi wa mradi
ngazi ya kitaifa kwa kufika mara kwa mara Mkoani Katavi kupokea changamoto
mbalimbali zinazowakabili watoto wenye ulemavu ambapo amesema kamati itaendelea
kutoa ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo
inayolea watoto wenye ulemavu wamesema uwepo wa mradi wa elimu Jumuishi Mkoani
Katavi umesaidia jamii kutambua haki za watoto wenye ulemavu ikiwemo kuwapeleka
shule na kuwapatia haki nyingine muhimu za kibinadamu.
Mradi wa elimu Jumuishi uliopo katika
mikoa ya Rukwa na Katavi pekee hapa nchini ulianza mwaka 2012 na unaratibiwa na
shirika la IFI lenye makao makuu Mkoani Arusha likijumuisha washirika watatu International
Centre on Disabilities(ICD),International Aid Services(IAS) na kanisa la Free Pentecosatl
Church Of Tanzania(FPCT).
Mtoa mada katika Kikao cha leo
ambacho kimefanyika katika Ofisi za mradi wa elimu Jumuishi Mjini Mpanda
alikuwa Bw.Verhan Bakari ambaye ni mshauri wa mradi wa elimu Jumuishi kutoka
Mkoani Arusha mradi ambao umesaidia kupatikana kwa haki za watoto wengi
waliokuwa wamenyimwa haki hasa suala la elimu kwa kufichwa majumbani.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments