WANANCHI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA KULIPWA FIDIA KABLA YA UPANUZI UWANJA WA NDEGE


Na.Issack Gerald
WIZARA ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano imewahakikishia kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka uwanja wa ndege Sumbawanga Mkoani Rukwa kabla ya kuanza upanuzi na ujenzi.
Uwanja wa ndege wa Sumbawanga kabla ya kuharibika
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa wizara hiyo Mh.Elias John Kwandikwa wakati akijibu swali la mbunge viti maalumu mkoani Rukwa Bupe Mwakang’ata aliyetaka kujua lini upanuzi na ujenzi wa uwanja wa ndege Sumbawanga utakamilika pamoja na kuwalipa fidia wananchi hao.
Amesema wananchi wa Sumbawanga waendelee kuvumilia kwani muda wowote watalipwa fidia na kuongeza kuwa sheria itazingatiwa ikiwa wananchi hawatalipwa fidia zao kwa wakati ili walipwe fidia ya ziada.
Aidha waziri Kwandikwa amesema mwezi Oktoba Mwaka 2016 serikali ilisaini mkataba na Kampuni ya SMPC kutoka Australia ili kusimamia ujenzi wa uwanja huo.
Wakati huohuo mwezi Juni mwaka huu,serikali ilitiliana saini mkataba na kampuni ya Sino Shine Over Seas Construction And Investment East Africa Limited kutoka nchini China ili kuanza ujenzi wa uwanja huo unaotarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 18 kuanzia mradi utakapoanza.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA