CHANGAMOTO SKIMU YA UMWAGILIAJI RUKWA, MKUU WA MKOA ATOA AGIZO KALI KWA WAFUGAJI WA MIFUGO

Na.Issack Gerald
MRADI wa skimu ya umwagiliaji ya Ng'ongo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa,unazidi kupungua uwezo wa kuzalisha mazao siku hadi siku kutokana na ukosefu wa maji pamoja na wafugaji wanaofuchungia mifugo katika eneo hilo.
Akizungungumza jana mbele ya mkuu wa mkoa wa Rukwa,mwenyekiti wa mradi wa scheme ya umwagiliaji ya Ng'ongo Justine Amon alisema kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 wakulima walilima hekta 128 na kufanikiwa kuzalisha tani 460.8 za mahindi.
Alisema katika msimu wa mwaka 2016/2017 katika hekta hizo 128 uzalidhaji umeshuka hadi kufikia tani 358.4 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo haribifu wa mazingira pamoja na wafugaji kuchungia ndani ya eneo la uzalishaji. 
Amon alisema eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 630 lakini zinazolimwa ni hizo 128 tu kwa kuwa ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 3,000 haujakamilika kwa muda mrefu sasa.
Mpaka sasa mfereji uliokalimilika unaurefu wa mita 1,725 ambao ndiyo unatumika katika umwagiliaji wa hekta hizo 128 ambazo wakulima wanafanya kilimo cha umwagiliaji mara mbili kwa mwaka ukitegemewa na vijiji vya Ng'ongo,Mwela na Mtowisa wakijishghulisha na kilimo cha mahindi,mpunga,nyanya na vitunguu.
Kwa mjibu wa mwenyekiti huyo,wakulima wangenufaika zaidi iwapo mradi huo ungekamilika kwani wapo baadhi ya wananchi wanatamani kulima wanashindwa kutokana na kutokamilika kwa mradi huo. 
Wahisani walitoa shilingi milioni 600 ili kujenga mradi huo uwanufaishe wananchi lakini walio wengi wameshindwa kunufaika kutokana na mradi huo kutokamilika kwa muda mrefu hivyo wanaiomba halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga itafute fedha ili kukamilisha mradi huo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesema ili uzalishaji uongezeka ni lazima sheria ndogo za halmashauri zitumike kuwabana waharibifu wa mazingira. 
Amesema bonde la ziwa Rukwa limeelemewa na mifugo maratatu zaidi ya uwezo wake na hivyo amewataka wafugaji wapunguze mifugo ambapo kwa atakayeshindwa kukubaliana na agizo lake basi aondoke mkoani Rukwa akatafute sehemu watakayo mpokea. 
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA