MWANAFUNZI WILAYANI TANGANYIKA AUWAWA KIKATIRI
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya
msingi Vikonge
Kata
ya tongwe wilaya ya Tanganyika mkoani katavi mwenye umri wa miaka
14 amefariki dunia baada ya kubakwa kisha kubakwa na kisha kutupwa
porini.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Katavi Damas Nyanda ameeleza kuwa tukio
hilo limetokea tarehe 22 majira ya saa mbili asubuhi wakati msichana huyo akiwa
na mdogo wake wa kiume kuelekea shuleni.
Ameongeza kusema upelelezi unaendelea ilikuwabaini walio husika na
kitendo hicho cha ukatili ili mkondo wa sheria uchukue nafasi yake.
Wananchi wamegadhabishwa na kitendo hicho
wengi wakilitaka jeshi la polisi kuwatia nguvuni wahalifu hao mara moja.
Katika hatua nyingine kamanda huyo amekemea
vikali kwa wale wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria akiwataka
kuzisalimisha jeshi la polisi.
Kwa mjibu wa kaka wa marehemu ambaye naye alikuwa mwanafunzi pamoja na
wakazi wa kijiji cha Vikonge wamesema kuwa mwanafunzi huyo aliomba lifti kwa
bodaboda na hivyo kubebwa ili kumrahishia kwenda shule ambapo baada ya hapo
alionekana akiwa amebakwa,kuchomwa kisu,kuuwawa na mwili kutelekezwa porini.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments