GESI YA HELIUM YA FUTI ZA UJAZO BILIONI 98.9 YAGUNDULIWA MKOANI RUKWA
Kampuni ya uchunguzi na utafiti wa madini Helium One, ambayo kwa sasa inafanya utafiti wa gesi ya heliamu mkoa wa Rukwa imegundua kuwapo kwa futi za ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo katika maeneo iliyokwishafanyia uchunguzi.
Hayo
yalielezwa katika warsha ya siku moja iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam
na kuratibiwa na Idara ya Jiolojia ya chuo hicho Helium One na Chuo Kikuu cha
Oxford.
Akizungumza
katika warsha hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Helium One,Thomas Abraham-James alisema
kampuni yao imetafuta leseni 23 za uchunguzi na kwamba nyingine tatu zimeombwa.
Alisema
leseni hizo zote zinamilikiwa na kampuni hiyo kwa asilimia 100 na kwamba ina
haki za kipekee za gesi hiyo ya heliamu .
Pamoja
na kutoa taarifa hiyo,alisema lengo la kuwa na warsha ni kuwaita wataalamu na
wadau mbalimbali wa hapa nchini na kimataifa kubadilishana uzoefu na taarifa
zilizopo kuhusu gesi hiyo na kuangalia fursa zinazoambatana na uwapo wa gesi
hiyo katika harakati za kitaifa za kuwa na taifa la viwanda.
Kwa
mujibu wa Abraham-James,warsha hiyo ilihudhuriwa na wanasayansi waandamizi wa
gesi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na Idara ya Jiolojia ya Chuo
Kikuu cha Dar es salaam,UDSM,watu wenye mamlaka na maamuzi,wadau wa maendeleo,watengeneza
sera kutoka serikalini,watafiti na sekta binafsi.
Aidha
kampuni hiyo imetoa ufadhili wa masomo ngazi ya shahada ya uzamili kwa
wanafunzi wawili wa UDSM kusoma katika Chuo Kikuu cha Oxford,ikiwa ni sehemu ya
kuingiza utaalamu wa hali ya juu wa kisayansi kwa watanzania na pia kuendeleza
uhusiano mzuri kati ya Helium One na UDSM.
Wakati
wa warsha hiyo,Profesa John Machiwa, akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo,Prof
Cuthbert Kimambo,alisema jukwaa hilo ni jema kwa wanafunzi, wakufunzi na Chuo
kizima kutafuta njia ya kuona namna ya kushirikiana na Helium One.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments