JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI KATAVI LAKIRI KUSHINDWAA KUWANASUA WALIONASA MGODINI
Miili ya vijana wawili waliofunikwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya dhahabu yaliyo kijiji cha Ibindi Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi bado haijaopolewa kwa wiki ya pili sasa.
Kwa upande wa mashuhuda wa ajali hilo katika eneo
la Kwa Songoro lililopo kijiji cha Ibindi wameelezea kusikitishwa na tukio hilo.
Kwa mujibu wa mashahidi mmoja ya vijana
waliopoteza maisha Azam Lawrence Nyembeke mkazi wa Iringa ndugu zake
hawana taarifa mpaka sasa.
Licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na
wachimbaji wakishirikiana na wananchi wa eneo hilo Jeshi la zimamoto na Uokoji
mkoani katavi limekiri kushindwa kutoa miili hiyo kwa madai ya
ukosefu wa vifaa kazi vinavyowezesha kurahisisha uokoaji huo.
Uchimbaji wa madini ni moja kati ya shughuli
ianyowakusanya vijana kutoka mikoa mbali nchini lakini wakiwa katika hatari
kubwa ya kupoteza maisha kutokana na teknolojia duni ya uchimbaji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments