MWANAFUNZI SUA ASAKWA KWA TUHUMA ZA KUMNYONGA MPENZI WAKE
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamsaka mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Mwita Marwa (30) kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga mpenzi wake Kibua Adam (39) baada ya kutokea kutokuelewana kati yao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Ulrich Matei amesema tukio hilo lilitokea Januari
22 mwaka huu katika eneo la Modeco Manispaa ya Morogoro ambapo mwanafunzi huyo
alitoweka baada ya tukio hilo.
Amesema
siku ya tukio mwanafunzi huyo na mpenzi wake ambaye ni mhudumu wa baa
walichukua chumba katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Aluta ambapo
walilala lakini baadaye mwili wa marehemu ulikutwa chumbani.
Hata
hivyo,kamanda huyo amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alimwandikia ujumbe wa
simu dada wa marehemu aitwaye Happiness Adamu ujumbe akisema kwamba tayari
marehemu keshatangulia na yeye mtuhumiwa atafuata.
Hata
hivyo,watu wa karibu wa marehemu ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema
marehemu alikuwa na mpenzi mwingine kabla ya Mwita na walipokorofishana ndipo
alipoamua kuwa na Mwita lakini siku chache kabla ya tukio alimwambia Mwita
kwamba mpenzi wake wa awali amejirekebisha hivyo anataka kurejeana naye jambo
ambalo mtuhumiwa alikuwa analipinga.
Kamanda
Matei amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya
Morogoro na jeshi hilo bado linaendelea na jitihada za kumsaka mtuhumiwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments