UHARIFU MTANDAONI SASA MPAKA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA
Wananchi Wilayani Mpanda Mkoani
Katavi wametakiwa kuwa makini wanapofanya miamala yoyote ya pesa kwa watu
wasiowafahamu vizuri ili kutokomeza utapeli wa pesa kimtandao ambao umeshamiri
Mkoani Katavi.
Wito huo umetolewa na Afisa wa Polisi
kutoka Ofisi ya Upelelezi Wilayani Mpanda Thobias Lindege ambapo ametoa elimu
ya kupambana na uharifu wa kimtandao elimu ambayo ameitoa kupitia baraza
maalumu la madiwani la Manispaa ya Mpanda.
Aidha Lindege amewataka wananchi
Mkoani Katavi kutonunua simu ovyo kutoka kwa watu bila utaratibu kwa kuwa
inapobainika simu hiyo imetumika kiuharifu,aliyenunua simu hiyo naye
huambatanishwa kama mharifu na hivyo kuwajibika katika kosa lililotendeka.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo amesema wanatarajia kufuatalia wa matangazo
yanayobandikwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda yakiwemo
yanayohusisha waganga wa jadi lengo likiwa ni kutokomeza utapeli katika
Manispaa ya Mpanda.
Baadhi ya njia ambazo zimetajwa
kutumiwa na matapeli ni pamoja na kupitia simu,ana kwa ana na benki ambapo
utapeli mkubwa kwa kiasi kikubwa unahusisha fedha.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments