RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME USO KWA USO NA TRUMP
Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia
kukutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa masuala ya kiuchumi
World Economic Forum (WEF) unaofanyika mjini Davos Uswizi.
Kagame atakuwa kiongozi wa pekee wa bara Afrika anayetarajiwa
kukutana na Trump kulingana na ratiba iliyotolewa na mshauri wa masuala ya
kiusalama wa Marekani H.R McMaster.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Ijumaa huku
kukiwa na malalamishi makubwa dhidi ya Trump ambaye aliyataja mataifa ya Afrika
kuwa machafu ambapo hata hivyo Trump Mwenyewe baadaye alikana madai hayo.
Mkutano wa rais Trump na Kagame ambaye
ndiye mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika utaimarisha uhusiano wa Afrika na
Marekani na kuzungumzia masuala muhimu ikiwemo biashara na usalama.
Muungano wa Afrika umemtaka rais Trump kuomba msamaha kwa
matamshi yake ya kukera ambapo wakati huo huo Trump anatarajiwa kukutana na
waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na rais wa Israel Benjamin Netanyahu mjini
Davos.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments