MFAHAMU RAIS JACOB ZUMA AMBAYE AMEJIUZULU URAIS
KIJANA
NA MWANAHARAKATI WA ANC
Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini
katika eneo la Kwa Zulu-Natal.Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga
na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya apartheid(ubaguzi
wa rangi wa kisheria).
Mwaka 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko Robben Island pamoja
na Nelson Mandela ambapo baada ya kuondoka
gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC
huko Msumbiji na Zambia na aliingia
katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC.
KUPANDA
NGAZI KATIKA AFRIKA KUSINI HURU
Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika
Kusini mwaka 1990,Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha Natal na baada ya
uchaguzi wa 1994 akawa waziri katika serikali ya jimbo.
Mwaka 1997 alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa
ANC na mwaka 1999 akateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri.
KUACHISHWA
KAZI SERIKALINI 2005
Mwaka 2005 mshauri wake Shabir Shaik
alihukumiwa miaka 15 jela kwa sababu alipokea rushwa.Zuma alishtakiwa pia na
Rais Thabo Mbeki akamwachisha Umakamu wa Rais.Kesi hii ilisimamishwa kwa sababu
mashitaka hayakuandaliwa vizuri.Kuna maandalizi ya kupeleka mashitaka mapya.
Miezi michache baadaye alishtakiwa tena kwa
sababu mama mmoja alidai ya kuwa alinajisiwa na Zuma.Katika kesi hii Zuma
hakuhukumiwa kwa sababu hakimu aliamini madai kwamba mama yule alikubaliana
naye.
KURUDI
KWAKE KAMA KIONGOZI WA ANC 2007
Mwaka 2007 Zuma akagombea nafasi ya
mwenyekiti wa ANC dhidi ya Thabo Mbeki aliyetaka
kuchaguliwa tena ambapo Zuma alishinda.
Na sasa tayari amejiuzulu urais leo Februari 15 baada ya kuandamwa sana na
chama chake.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments