MORGAN TSVANGIRAI AFARIKI DUNIA
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan
Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.
Kwa
mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC,Tsvangirai mwenye umri wa 65,na
aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa
alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.
Makamu
Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri amesema marehemu alifariki jana jioni
Februar 14.
Katika
kipindi cha uhai wake,maisha yake ya kazi yaligubikwa na harakati nyingi za
kisiasa dhidi ya mpinzani wake Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Morgan
Tsvangirai alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC- mwaka 2000
na kuanza kutoa changamoto kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyekaa madarakani
muda mrefu.
Kufuatia
kifo hicho Bw.Tsvangirai,MDC inaelekea kugawanyika juu ya nani atakayeongoza
uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa
sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa.
Bw.Tsvangirai,Aliwahi kupigwa na kufungwa
mara kadhaa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments