HATIMAYE RAIS ZUMA AJIUZULU
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
ameamua kujiuzulu mara moja kufuatia kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa chama
chake kinachotawala nchini humo cha African National Congress, ANC.
Afisa
mmoja mwandamizi wa chama hicho amesema hatua hiyo italeta utulivu wakati nchi
inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Ameongeza kwa kusema kuwa ANC
haisherehekei hatua hiyo,kutokana na kuwa Zuma amekitumikia chama hicho kwa
miaka 60.
Awali
kupitia televisheni Bw.Zuma alisema hakubaliani na mahitaji ya uongozi wa ANC
kwamba anapaswa kujiuzulu, lakini amejiuzulu ili kuepusha ghasia ambazo
zingechafua jina lake.
Makamu
wa Rais wa Africa kusini Cyril Ramaphosa atapigiwa kura na wabunge kama mkuu wa
nchi na baadaye kula kiapo ndani ya siku chache zijazo.
Zuma alikilalamikia chama cha ANC kwa kumtaka aondoke
madarakani,ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuondoa kupitia kura ya bunge ya
kutokuwa na imani naye iliyopangwa kupigwa hii leo Alhamisi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments