RAIS JACOB ZUMA ASEMA HAONI SABABU YOYOTE YA KUJIUZULU
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema hajafanya makosa na haoni sababu ya kujiuzulu.
Bw.Zuma
alizungumza baada ya chama tawala cha ANC kumtaka kujiuzulu vinginevyo
atakabiliwa na kura isiokuwa na imani dhidi yake leo Alhamisi.
Rais
huyo amekuwa chini ya shinikizo ya kujiuzulu huku kukiwa na madai mengi ya
ufisadi lakini amesema ANC imeshindwa kuelezea ni kwa nini ametakiwa kujiuzulu.
Bw.Zuma amesema yuko tayari kuondoka
baada ya mwezi Juni lakini akapinga vile jambo hilo linavyoangaziwa kwa sasa na
alisema atatoa taarifa nyengine baadaye siku ya Jumatano.
Chama
cha ANC kimesema kilisikiza matamshi ya Bw.Zuma lakini kitatoa uamuzi wa hatua
yake baadaye kabla ya kuzungumza.
Kiongozi
wa chama hicho Jackson Mthembu alitangaza kuwa kura isiokuwa na imani dhidi ya
rais itasikilizwa siku ya Alhamisi huku Cyril Ramaphosa aliyechaguliwa kuwa
rais wa chama hicho mwezi Disemba akiapishwa mara moja kuwa rais wa taifa hilo.
Mkutano
wa kamati kuu ya ANC ulikuwa umetangaza uamuzi wake wa kumtaka Zuma ajiuzulu
siku ya Jumanne na kumpatia hadi mwisho wa siku siku ya Jumatano kujiuzulu.
Katika mahojiano,bw.Zuma hakuzungumza
kuhusu uvamizi wa mapema alfajiri uliotekelezwa na maafisa wa polisi katika
nyumba ya washirika wake wakuu familia ya Gupta siku ya Jumatano.
Familia
ya Gupta imetuhumiwa kwa kutumia uhusiano wa karibu na rais kuwa na ushawishi
mkubwa wa kisiasa ambapo hata hivyo pande zote mbili zimekataa kuwepo kwa madai
hayo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments