MWANAFUNZI ALIYEPOTEA TANZANIA APATIKANA AKIWA HAJITAMBUI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akiongea na waandishi wa habari kuelezea tukio la kupatikana kwa Mwananchuo Abdul Nondo |
Inadaiwa
kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la
usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao
walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha
polisi kilichoko karibu.
Mahojiano
yake katika kituo cha Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye
kupiga simu kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe,baba
mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua
nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana
na kutekwa kwake.
Alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne
katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa
ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini
humo,Tahliso.
Mtandao
wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ulisema baada ya kuondoka afisi hizo, Bw Nondo
alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale.
Awali
kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara
kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa
usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.
Jeshi la Polisi Mkoani
Iringa limeeleza kuwa limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omari Nondo
alikuwa ametekwa au la ili liweze kuwachukulia hatua za kisheria wote
waliohusika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Chanzo:bbc
Comments