MAHAKAMA KUU IMETENGUWA KUFUKUZWA WABUNGE 8 NA MADIWANI 2 WA CUFU
Mahakama
Kuu leo imetengua kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananchi,CUF na
kusitisha pia mchakato wa kuwafukuza uanachama mpaka shauri la msingi
litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
Aidha Mahakama hiyo pia imemzuia Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa,Prof.Ibrahim Haruna Lipumba,
Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF kujadili kuhusu uanachama wa
Wabunge na Madiwani hao.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na
Mahusiano Na Umma ya CUF Taifa, imeeleza kuwa, Mahakama Kuu imekubaliana na
Hoja za Wabunge 8 wa chama hicho na imeona hoja za msingi za madai yao
zinazopaswa kuangaliwa kuhusu uhalali wa masuala yote yaliyowasilishwa mbele ya
Mahakama hiyo.
Imefafanua kwamba, Mahakama Kuu pia imeyatupilia mbali
mapingamizi mengine yote yaliyowekwa na Prof. Lipumba na Wenzake katika shauri
hilo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments