RAIS MAGUFULI AWATAKA TAKUKURU KUTOKUWA NA KIGUGUMIZI DHIDI YA WAHUSIKA VITENDO VYA WA RUSHWA-Agosti 28,2017
Rais Magufuli akiwa ndani ya Ofisi ya Takukulu |
Mhe. Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipotembelea na
kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi
hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais
Magufuli amesema ana imani na TAKUKURU na amewataka wafanyakazi wa taasisi hiyo
kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu mkubwa na kwamba
Serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano
huo Mhe. Rais Magufuli amepokea masuala mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa
TAKUKURU na amewaahidi kuwa Serikali itayafanyia kazi ili kuboresha maslahi yao
na mazingira ya kazi.
Mkutano huo
umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Katibu Mkuu Dkt. Laurian Ndumbaro na
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi
na wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa mradi
wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Hydropower
Project), ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha
kisasa (Standard Gauge) na ujenzi wa barabara mbalimbali nchini, Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Katika Mkutano
huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Matogolo Kalemani ametoa
taarifa ya maandalizi ya awali ya kuanza kwa ujenzi wa mradi wa umeme wa
Stiegler’ Gorge na kwamba zabuni ya kuanza kwa ujenzi huo itatangazwa tarehe 30
Agosti, 2017.
Mhe. Rais
Magufuli amesema fedha za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa utakaozalisha
Megawatts 2,100 zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa zipo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments