UCHAGUZI MWENYEKITI HALMASHAULI YA BUHIGWE MIZENGWE MITUPU-HALMASHAURI IMEZUNGUMZA
Baraza la madiwani wilayani Buhigwe mkoani kigoma, limeshindwa
kumchagua mwenyekiti wa halmashauri hiyo, baada ya kikao kilichotakiwa
kufanyika kwa ajili ya kumchaguwa mwenyekiti kuahirishwa kutokana na
kutokuzingatiwa kwa taratibu za uchaguzi.
Uchaguzi wa mwenyekiti huyo ulitakiwa kufanyika October 21, ambapo
mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Bw.Anoster Nyamoga,alichelewa kufika katika
kikao hicho ambapo alifika mnamo saa tisa alasiri badara ya saa nne asubuhi
kama mwaliko ulivyokuwa unaeleza , ambapo aliwaomba radhi madiwani hao, na
kusema kuwa alikuwa katika majukum mengine ikiwa ni pamoja na vikao vya chama
cha mapinduzi.
Kabla ya kikao kufunguliwa Diwani wa viti maalum , tarafa ya
manyovu Bi,Eles Gomwa, aliomba mwongozo kwa ajili ya kuahilisha kikao hicho,
ambapo aliomba kufanyika kwa vikao vya kuvunja kamati kwanza ,na hatimaye
uchaguzi uweze kufanyika, ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zingine
ambazo zilionekana hazijakamilika katika uchaguzi huo.
Aidha kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Bw.Wilson
Rusibila,alikiri kuwa taratibu za uchaguzi huo haikufuatwa na kuridhia
kuahilishwa kwa kkao hicho na kusema kuwa taratibu za kuandaa baraza zitaanza
upya ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza katika kikao kingine
kitakachopangwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments