RAIS MAGUFULI AMETEUA GAVANA MPYA WA BENKI KUU YA TANZANIA(BOT) PIA ANGALIA ORODHA YA WAJUMBE WALIOPATA TUZO SUALA LA MAKINIKIA

Na.Issack Gerald
Prof.Frorens Luoga Gavana Mpya BOT
Rais John Magufuli amemteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kuchukua nafasi ya Profesa Benno Ndullu anayemaliza muda wake.
Rais Magufuli ametangaza uteuzi huo leo akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kutoa vyeti kwa kamati zilizohusika na ripoti za madini nchini.
Akizungumza baada ya kutoa vyeti hivyo amesema atamteua gavana kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashauriano kuhusu madini kutokana na kuridhishwa na kazi yao.
Gavana Beno Ndullu,ambaye amekuwa Gavana wa BOT tangu 2008 anamaliza muda wake ifikapo mwezi Januari mwakani.
Huo ni uteuzi wa pili kwa Profesa Luoga,kwani Julai 11 mwaka huu Rais Magufuli alimteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA).
Profesa Luoga alichukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa.
ORODHA WALIOTUNUKIWA VYETI
1.Jobu Yusto Ndugai(Spika wa Bunge Tanzania)
2.Prof.Nehemia Eliakim Osolo
3.Prof.Abdulkarim Hamis Mruma
4.James Dotto Mgosha
5.Dkt.Yamungu Mahwago Kayandabila
6.Geofrey Mwambe
7.Adolfu Yasini Kitungulu
8.Prof.Frorence Dominick Andrea Makinyika Luoga
9.Kasmiri Sumba Kiuki
10.Andrea Wilison Masawe
11.Saje Bernad Asubibisye
12.Ade Jemmy Andangwile Mwaipopo
13.Eddy France Sikuluasha
14.Moses Edward Moses
15.Roya John Lianga
16.Andea Abraham Mwangakala
17.Michael Jonathan Kambi
18.Prof.Longinus Kyaluzi Lutasikala
19.Dkt Osward Joseph Mashindano
20.Gabriel Paschal Malata
21.Butamo Kasuka Philip
22.Prof.Justine Zahula Ikingula
23.Prof.Joseph Rogasila Buchweshaija
24.Dkt.Othman Yusuph Ngenya
25.Dkt.Joseph Yoeza Philip
26.Dkt Ambrose Joseph Matoro Ikika
27.Mohamed Zeno Makongolo
28.Heri Issa Gombera


Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA