WAZIRI LUKUVI AFAFANUA ZAIDI KUHUSU BOMOABOMOA NCHINI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameyasema hayo ametoa ufafanuzi kuhusu uwekaji wa alama za X na kuvunja majengo yanayojengwa katika miji bila kibali.
Waziri Lukuvi ametoa ufafanuzi huo leo ikulu wakati rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango aina na thamani ya madini katika makinikia.
Amesema zoezi hilo litakuwa sambamba na kuwaondoa wavamizi katika viwanja vya watu waliowadhulumu watu wengine walio na hati miliki za ardhi na kujenga nyumba zao.
Aidha Lukuvi amesema viongozi wote wa wilaya na mitaa wahamasishe wananchi kushiriki kikamilifu katika urasimishaji wa makazi yao kwa faida yao na Taifa kwa jumla.
Waziri Lukuvi alitoa agizo hilo jana Oktoba 22 2017 ambapo aliwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri,Maafisa Ardhi,Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka alama za X na kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao bila kibali na yale yanayojengwa katika viwanja vya watu wengine walio na hati.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA