MKAZI MMOJA MKOANI KATAVI AMENUSURIKA KUUWAWA USIKU WA KUAMKIA LEO
Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la
James Modest mkazi wa Kijiji cha Mnyaki A kata ya Katumba Wilayani Mpanda amenusurika kuuwawa baada ya watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.
Kwa mjibu wa James Modest ambaye ni
Mhanga wa tukio hilo amesema ameporwa fedha taslimu shilingi 730,000 vifaa vya
sola za umeme vyenye thamani ya shilingi 70,000.
Aidha amesema ndani waliingia watu
watatu na kuanza kumshambulia kwa vitu vizito ambapo walichukua kiasi hicho cha
fedha na kumuamru awakabidhi simu ya Smartphone yenye thamani ya 220,000
pamoja,simu ndogo yenye thamani ya shilingi 40000.
Shuhuda wa tukio hilo Yadunia Modest ambaye
pia ni kaka wa aliyejeruhiwa na kuporwa mali zake,amesema mdogo wake
amekatwakatwa kwa mapanga na kujeruhiwa puani na kichwani hali ambayo
imemsababishia maumivu makali.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mnyaki A
Bw.Kisele Meshack amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa tukipo hilo limetokea
usiku wa kuamka leo,majira ya saa 7 ambapo amesema majeruhi alipatiwa matibabu
katika kituo cha afya Katumba na kuruhusiwa.
Tukio
hilo linatajwa kuwa miongoni mwa matukio manne ya kutoka katika kijiji cha
Mnyaki kata ya Katumba ambapo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Oktoba
mwaka huu hakuna mauaji yaliyotokea bali uporaji wa mali na watu kujeruhiwa.
Kwa
takribani wiki mbili zilizopita,kumekuwa na mfululizo wa watu kuvamiwa majumbani
na kuibiwa mali ikiwemo wengine kuuwawa.
Miongoni
mwa matukio hayo ni pamoja na tukio lililotokea Oktoba 12 mwaka huu ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jila la Suzani Chales (40) mkaazi
wa Kata ya Katuma wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi alikufa kwa kupigwa risasi
na watu wasiojulikana.
Comments