TFS WAMETOA ONYO KWA WAVAMIZI WA HIFADHI ZA MISITU MKOANI KATAVI
Wakazi mkoani katavi wametakiwa kuacha tabia ya kuvamia
misitu na kufanya shughuli katika hifadhi zinazoharibu uoto wa asili.
Kauli hiyo imetolewa na Samwel Matula ambaye meneja wa
misitu (TFS) kanda maalum ya mkoa wa Katavi ambapo amesema hakuna ruhusa ya
watu kufanya shughuli kama kilimo au kuweka makazi katika hifadhi zilizopo
katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo meneja misitu wilaya ya mpanda Mustafa Abedi
amewataka wote walioondolewa katika maeneo ya misitu kufuatia operesheni
iliyofanyika mwezi wa saba mwaka huu ,kutorudi katika maeneo hayo na sheria
kali zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo.
Mwezi Julai mwaka
huu,operesheni ya kuwaondoa watu katika maeneo ya misitu kama vile msitu wa
msaginya ,na misitu north east mpanda ilifanyika kwa lengo la kulinda misitu
iliyopo Katavi kwa manufaa ya wananchi wote.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments