MH.ZITTO AMEPEWA DHAMANA
Mbunge
wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa
dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa Mkurugenzi wa
upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria
wa Zitto Kabwe amesema mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa mawili
tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya mitandao lakini kosa
jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 37 (5) cha sheria ya
takwimu ya mwaka 2015.
Mwanasheria
amesema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri kujua kama
watakwenda mahakamani.
Kwa
upande wake Zitto Kabwe amesema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa
mahakamani ili kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa ambayo wanayaona
kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua vizuri ni mahakamani na
kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa kuwa tayari Rais alikuwa
ameshatoa agizo.
Mbali
na hilo kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka wanachama pamoja na viongozi wa
chama hicho kuendelea na harakati za uchaguzi mdogo wa udiwani na kusema endapo
wakishinda katika uchaguzi huo ni kitu ambacho kitakuwa faraja kwao.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments