VIWANDA VYA MWATEX NA KEKO VIMEPEWA SIKU 14 VIZALISHE BIDHAA
Rais
John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa kiwanda cha nguo cha Mwatex cha
jijini Mwanza na cha dawa cha Keko jijini Dar es Salaam kuanza uendeshaji wa
kiuzalishaji.
Rais
Magufuli amesema hayo jana alipozungumza na wananchi baada ya kuzindua kiwanda
cha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical eneo la Buhongwa jijini Mwanza.
Amesema
Serikali imechoka kusikia kauli na maelezo ya “tuko kwenye mchakato”
zinazotolewa kama kinga kwa viwanda visivyofanya kazi kwa kiwango
kinachostahili.
Rais
ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa kiwanda cha Mwatex kinafanya
kazi kwa asilimia 20 ya uwezo wake wa uzalishaji.
Akizungumzia
ujenzi wa kiwanda cha dawa,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto
Ummy Mwalimu amesema utawezesha mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwa na uhakika wa
upatikanaji wa dawa kwa bei nafuu.
Mwalimu
amesema katika utekelezaji wa Tanzania ya viwanda,wizara kwa kushirikiana na
wadau wanakamilisha mchakato wa kujenga kiwanda cha dripu na bidhaa zingine za
hospitali mkoani Simiyu.
Kuhusu
uboreshaji wa huduma za afya,amesema Mkoa wa Mwanza umepokea zaidi ya Sh7.1
bilioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba na dawa.
Amesema
jitihada zinaendelea ili kuipatia Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou-Toure
mashine ya CT-Scan.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments