MASOKO YA USIKU MKOANI KIGOMA,HOFU USALAMA IMETANDA
Imeelezwa kuwa Masoko
ya usiku katika baadhi ya kata za wilaya ya Buhigwe mkoani kigoma,yanapalekea
matatizo kwa wakazi wa wilaya hiyo,yakiwemo matatizo ya kiusalama kutokana na
wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi jirani ya Burundi.
Diwani wa kata ya Mkatanga
ambaye ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe,Bw.Hamiss
Lukanka amesema soko hasa lililoko katika kata ya Mkatanga linapelekea
hata watoto wa shule kutokupata muda wa kujisomea kutokana kutumia muda wao
mwingi hasa wa usiku kuzurula sokoni humo.
Amesema mpaka sasa wana
mpango wa kuratibu na kusimamia soko hilo liwe linaanza muda wa asubuhi kwa
siku maalum,ili kuondokana na changamoto zinazotokana na masoko ya usiku na
kutoa nafasi kwa wakazi wa vijiji jirani kuleta bidhaa zao katika soko hilo.
Katika upande mwingine
Bw.Lukanka amewataka wananchi wa wilaya ya Buhigwe kufanya kazi kwa
kushilikiana Bila kujali utofauti wa vyama wilayani humo,lengo kubwa
likiwa ni kuleta maendeleo ya wilaya yao.
Chanzo:Grol
Paschal,Mhariri-Issack Gerald
Comments