MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA AMERUHUSU AJIRA ZA MUDA
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ameagiza kuajiriwa kwa baadhi ya maafisa kata wa muda katika baadhi ya Kata.
Amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda alipokuwa akijibu
baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Waheshimiwa madiwani kuhusu tatizo hilo.
Katika hatua nyingine amezitaja baadhi ya sababu
zilizopelekea upungufu wa watendaji hao kuwa ni baadhi yao kukumbwa na sakata
la watumishi wenye vyeti feki.
Wiki iliyopita Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Bi.Lilian Matinga alitoa agizo kwa vijiji na mitaa kuajiri watumishi wa
muda wakati wakisubiri serikali kuu kutangaza ajira.
Baraza la Madiwani limeendelea jana ambapo Madiwani
wamewasilisha mapendekezo mbalimbali ya utekelezwaji wa bajeti katika kata zao.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments