TMA YATOA ANGALIZO
Mamlaka ya hali ya hewa nchini imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa mvua kubwa katika baadhi ya mikoa ya Rukwa, Mbeya,Songwe,Iringa,Njombe na Ruvuma kuanzia leo usiku.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo
jioni ya leo na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya upepo mkali unaozidi
kilomita 40 kwa saa.
Aidha taarifa hiyo inaonesha mawimbi makubwa yanayozidi mita
2 vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam,Pwani,Lindi,Mtwara
pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Comments