HABARI PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA FEBRUARI 7,2018

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kutekeleza dhana ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda.
Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjelina Mabula akisisistiza umuhimu wa Halmashauri kutenga maeneo ambayo yatatumiwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kujenga nyumba za gharama nafuu zitakazouzwa kwa wananchi na watumishi wa Halamshauri husika.
Mbunge wa Urambo Mashariki Mhe. Magreth Sita akiuliza Swali Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutatua migogoro ya Ardhi ikiwemo kubatilisha matumizi ya mashamba ambayo hayajaendelezwa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Aderladus Kilangi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati hiyo kwa mwaka 2017/2018.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisisitiza jambo kwa wabunge nje ya Viwanja vya Bunge mapema leo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA