DC AKABIDHI GARI LA KUZOA TAKA


MKUU wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi.Lilian Charles Matinga,amekabidhi lori jipya la kuzoa taka katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

Bi.Matinga mbali na kuwapongeza Halmashauri kwa kununua gari hilo,ametaka gari hilo litumike kwa ajili ya kufanya usafi kwa kuzoa taka kama lilivyokusudiwa.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Wilium Mbogo mara baada ya kukabidhiwa gari hilo,amesema gari hilo limetokana na fedha ambazo zilikuwa zimepangwa kutumika kununua gari la la Meya ambapo amewapongeza baraza la madiwani kwa kubadili matumizi hayo kwa ajili ya maslahi ya Halmashauri.

Naye Kaimu mkuruingenzi wa Manispaa ya Mpanda Deodatus Kangu, amesema shilingi milioni 159 zilizotumika kununua gari hilo zimetokana na makusanyo ya ndani ya manispaa na amesema kuwa litasaidia kuzoa taka kwa wakati.

Kwa mjibu wa takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na maafisa afya wa Manispaa ya Mpanda huzalisha kiasi cha taka tani 70.5 kila siku ambapo kununuliwa kwa lori hilo lenye uwezo wa kubeba tani 16 litaondoa mrundikano wa taka katika vizimba mbalimbali vilivyojengwa katika Manispaa.

Mara kwa mara wananchi wamekuwa wakilalamika taka kurundikana kwa muda mrefu katika makazi yao huku wakielezea kuhofia magonjwa ya mlipuko hasa wakati wa masika ambapo kunakuwa na uozo wa taka.
Chanzo:Manispaa ya Mpanda

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA