BEI MPYA YA MAFUTA INAYOANZA KOTE KUTUMIKA NCHINI
Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta
zinazoanza kutumika leo Februari 7 huku bei za petroli,dizeli na mafuta ya taa
zikipanda.
Taarifa
ambayo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Nzinyangwa Mchany amesema
bei za rejareja zimeongezeka kwa petroli ikiwa ni Sh59 sawa na 2.70%,dizeli
Sh46 sawa na 2.30%,na mafuta ya taa kwa Sh24 sawa na 1.17%.
Wakati
huo huo amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambao kwa petroli ni Shilingi 58.57
sawa na 2.85%,dizeli kwa Shilingi 46.48 sawa na 2.44% na mafuta ya taa kwa Shilingi
23.75 sawa na 1.24%.
Amesema
bei za rejareja katika mikoa ya Kaskazini zimeongezeka,ambapo petroli ni kwa Shilingi15
sawa na 0.70% na dizeli kwa Shilingi 47 sawa na 2.29%.
Kwa
upande wa Bei za jumla zimeongezeka petroli ikiwa ni kwa Shilingi 15.36 sawa na
0.73% na dizeli Shilingi 47.18 sawa na 2.42%.
Katika
hatua nyingine Mchany amesema sehemu ya shehena kubwa ya mafuta yaliyopokelewa
katika Bandari ya Dar es Salaam ni yenye bei ya soko la dunia za Novemba,2017
wakati iliyopokewa katika Bandari ya Tanga ni ya bei ya soko la dunia ya
Desemba 2017.
Amebainisha
kuwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya
asilimia 6 ikilinganishwa na bei za Oktoba 2017 wakati bei za Desemba zina
mabadiliko tofauti.
Amesema
bei ya petroli imepungua kwa asilimia 0.2 na ya dizeli na mafuta ya taa imeongezeka
kwa asilimia 2.7 na asilimia 1.9.
Comments