JAJI MKUU WA KENYA AILAUMU SERIKALI YAKE KUKIUKA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI
Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga
ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha sheria na
katiba ya kenya katika kukabiliana na upinzani.
Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga |
Tamko hilo limekuja mara tu baada ya
kiongozi mmoja wa upinzani wakili Miguna Miguna kufukuziwa nchini Canada,baada
ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano hata baada ya mahakama kutoa amri kwamba
aachiliwe kwa dhamana .
Katika maelezo yake jaji David Maraga,amesema
malalamiko yaliyopelewekwa mahakamani yalikuwa wazi,na yalikuwa majukumu ya
mahakama kufanya maamuzi kwa kuwa ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila
mmoja pamoja na serikali yenyewe.
Jaji huyo ametoa tamko hilo la
kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya
kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama.
Kwa mjibu wa madai ya serikali ya
Kenya ni Kwamba Miguna Miguna alishakana uraia wa Kenya na kuchukua uraia wa
Canada ambapo kata hivyo kwa mjibu wa katiba ya Kenya raia wan chi hiyo
anaruhusiwa kuwa na u8raia wan chi mbili.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments