MKOANI KATAVI AHUKUMIWA JELA KWA KUMILIKI RISASI ZA SILAHA YA KIVITA
Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoani
Katavi imetoa hukumu dhidi ya Bw.Kigalu Huba(25) mkazi wa kijiji cha Kambuzi
wilayani Mpanda Mkoani Katavi aliyekuwa akituhumiwa kwa kosa la kukutwa na risasi
12 za silaha AK-47 ya kivita ambapo mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka
20.
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mh.Chiganga Tengwa akitoa hukumu hiyo leo
amesema mahakama imejiridhisha bila kuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo baada
ya kusikiliza shadi wa pande zote ambazo ni mtuhumiwa na upande wa Jamhuri
ambao ni serikali.
Awali upande wa Jamhuri ambayo ni
serikali wamesema Bw. Kigalu Huba alikutwa na risasi hizo Machi 19,2018 ambapo
ni kinyume na kifungu cha sheria namba 7 ya mwaka 2015 kinachohusu umiliki wa
silaha huku wakiiomba Mahakam itowe
adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe wenye tabia kama hiyo.
Kwa upande wake Bw.Huba akitoa
utetezi wake mahakamani hapo ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu aliyopewa
akisema kuwa anategewa ana mke na watoto watatu na asipopunguziwa adhabau hiyo familia
yake itaathirika.
Aidha katika maelezo ya mtuhumiwa ni
kuwa risasi hizo hazikuwa zake bali zilikuwa na mwananchi mwingine ambaye
amemtaja kwa jina moja la Shimangu anayeishi katika kijiji ambacho yeye
Bw.Kigalu Huba hakifahamu kwa kuwa walikuwa wanakutana miataani.
Mara baada ya utetezi huo baada ya
mahakama imejiridhisha kujirisha bila shaka kuwa ni mtuhumiwa alitenda kosa
hilo ambapo hakimu Mh.Chgangwa Tengwa kwa kuzingatia kifungu cha 235(1) ya mwenendo
ya makosa jinai sheria namba 20 ya mwaka 2002 amemhukumu kwenda jera miaka 20
kuanzia Aprili 10,2018.
Kwa mjibu wa hukumu hiyo,mtuhumiwa ana
nafasi ya kukata rufaa ikiwapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa dhidi yake
kutokana na mashtaka yanayomkabili.
Nao baadhi ya wananchi kutoka kijiji
cha Kambuzi walikuwa wamehudhuria ili kufahamu hatima ya kesi ya Bw.Kigalu Huba
ambaye wamekuwa wakimtuhumu kuwa tishio kwa wananchi kwa kujihusisha na
uharifu.
Katika kesi hiyo Mashuhuda wapatao wane
walihudhuria kutoa ushahidi akiwemo mkuu wa upelelezi kutoka jeshi la Polisi
Mkoani Katavi Emmanuel Parangyo,wananchi pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha
Kambuzi Halt ambao walithibitisha mtuhumiwa kukutwa na risasi hizo 12 zikiwa
katika mfuko wa Rambo nyeusi katika nyumba aliyokuwa akiishi hapo kambuzi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments