CHADEMA WAZUNGUMZIA KIFO CHA KADA WAKE MKONGWE
Mwenekiti
wa Chadema taifa Mh.Freeman Mbowe ameeleza kusikitishwa na taarifa ya kifo cha
Tambwe Richard Hizza.
Amesema
kuwa Hizza alipotoka CCM na kwenda upinzani kwake yeye ni kama alikuwa anatubu
kwani hakutaka kufa akiwa ndani ya CCM.
Mbowe
amesema hayo jana Februari 8 baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Tambwe
Richard Hizza ambaye amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana.
Kufuatia
kifo cha Hizza Mwenyekiti wa CHADEMA amedai wao ili kumuenzi kamwe hawawezi
kurudi nyuma bali watasimamia yale wanayoyaamini ili kumuenzi na kufikia
matamanio ambayo kiongozi huyo alikuwa akiyatamani.
Hizza katika moja ya mikutano ya Chadema |
Richard Hizza amekuwa akishiriki katika kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo la
Kinondoni toka siku ya ufunguzi wa kampeni hizo Januari 27,2018 na siku moja
kabla ya kifo chake alishiriki kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge kupitia
CHADEMA.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments