HALMASHAURI YATOA TAHADHARI KWA WAZAZI KUPELEKA WATOTO KATIKA SHULE ZISIZOSAJILIWA
Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi imetoa tahadhari kwa wazazi Mkoani Katavi wanaowapeleka watoto
wao katika shule mbalimbali za Manispaa ambazo hazijasajiliwa.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu
taaluma Manispaa ya Mpanda Mwalimu Rashid Pili wakati akizungumza kuhusu uwepo
wa baadhi ya shule ambazo hazijasajiliwa lakini tayari zikiwa zimesajili
wanafunzi wa shule za msingi na chekechea.
Kwa mjibu wa Mwalimu Pili,Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda ina Shule 36 zikiwemo 34 za serikali na 2 za binafsi za
Reimeta na Nzela English Pre-Primary School zinazotambuliwa na serikali ambapo mtoto
anayesajiliwa nje ya shule hizo hatambuliki katika mfumo wa elimu Tanzania.
Hata hivyo Mwalimu Pili amesema
Ijumaa ya Wiki hii wanatarajia kukutana na wamiliki wa shule hizo ili kufikia
mwafaka ili kuendesha mambo kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni za nchi.
Aidha Mwalimu Pili amesema katika
mwaka 2018 manispaa ya Mpanda imejipanga kufaulisha kwa karibu asilimia 99 ili
kurejea katika nafasi ya kwanza iliyokuwa nayo katika kipindi cha mwaka
2016,2015 na 2014.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments