KENYATTA ATEUA MAWAZIRI WAPYA KENYA NA BALOZI MPYA TANZANIA
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake
mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana.
Rais Uhuru Kenyatta |
Mawaziri sita ambao walikuwa
wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa
kuwa mabalozi.
Bw.Dan Kazungu ambaye amekuwa waziri
wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania.
Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo
Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika
uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Miongoni mwa walioteuliwa kuwa
mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa
waziri wa ardhi.
Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na
Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la
Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva.
Bi.Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri
mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekezwa kuwa
waziri wa elimu.
Mawaziri walioteuliwa kuwa mabalozi
Judi Wakhungu (Mazingira) - Ufaransa
Cleopa Mailu (Afya) - Umoja wa
Mataifa mjini Geneva
Dan Kazungu (Madini) - Tanzania
Phylis Kandie (Leba na Jumuiya ya
Afrika Mashariki) - Ubelgiji, Luxemburg na Umoja wa Ulaya
Willy Bett (Kilimo) - India
Jacob Kaimenyi (Ardhi) -UNESCO, Paris
Hassan Wario (Michezo) - Austria
Kwa sasa, orodha kamili ya mawaziri
waliopendekezwa ni:
Adan Mohammed - Viwanda
Amina Mohammed - Elimu
Charles Keter - Kawi
Eugene Wamalwa - Ugatuzi
Farida Karoney - Ardhi
Fred Matiangi - Masuala ya Ndani na
Usalama
Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu)
James Macharia - Uchukuzi
John Munyes - Madini na Mafuta
Joseph Mucheru - Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano
Keriako Tobiko - Mazingira
Margaret Kobia - Vijana na Utumishi
wa Umma
Monica Juma -Mambo ya Nje
Mwangi Kiunjuri - Kilimo
Najib Balala - Utalii
Peter Munya - Jumuiya ya Afrika
Mashariki
Racheal Omamo - Ulinzi
Raphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa
sasa)
Rashid Achesa - Michezo
Sicily Kariuki - Afya
Simon Chergui - Maji
Ukur Yattany - Leba
Chanzo:bbc swahili
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments