MIMBA ZA UTOTONI BADO TATIZO KULIDHIBITI
Na.Issack Gerald
Tatizo la mimba za utotoni katika
kata Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi limekuwa gumu kulidhibiti
kutokana na jamii inayoishi mahali hapo kuishi kwa kuhamahama.
Hali hiyo imethibitishwa na Afisa
Mtendaji wa Kata ya Mwamkulu Bw.George Iresha wakati akizungumza kuhusu namna
wanavyodhibiti watoto wenye umri mdogo kupata mimba.
Aidha amesema kuongezeka kwa shule za
msingi na vituo shikizi vya kielimu katika kata ya mwamkulu imewapunguzia
mwendo mrefu watoto ambapo umbali mrefu kutoka nyumbani mpaka shule zilipo
zimekuwa zikitajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyochangia mimba za utotoni.
Kata ya mwamkulu yenye wakazi wapatao
elfu saba ikiwa na wakazi wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji ni miongoni
mwa kata 15 za manispaa ya Mpanda.
Mpaka sasa Mkoa wa Katavi unaongoza
asilimia 45 kwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kati ya Mikoa yote
Tanzania.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments