HAKIMU ATAKA WATENDAJI WA MAHAKAMA WAWAJIBIKE KWA MJIBU WA SHERIA
Hakimu mfawidhi wa mahakama
ya mkoa wa Katavi Hassan Omary amewataka watendaji wa mahakama kusimamia
maadili ya kazi zao katika uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi katika kutoa
maamuzi mbalimbali ya kesi wanazoziendesha ktika maeneo yao yakazi.
Bw.Omary amesema kuna baadhi
ya malalamiko ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wananchi yanayowalenga moja
kwa moja baadhi ya watumishi wa mahakama katika utekelezaji wa majukumu yao kwa
wananchi hasa yale ya ucheleweshwaji wa maauzi ya kesi pasipo na sababu za
msingi
Aidha amesisitiza kuwa
nivyema wanachi kufahamu kuwa mahakama ndiyo sehemu sahihi ya kukimbilia pindi
wanapoona haki zao zinapolwa na watu wasio jua taratibu kanuni na sheria za
nchi pamoja na hayo amesema muhimili huo wa utoaji haki nivyema ukaachwa
ufanyekazi yake pasipokuingiliwa na Mtu au taasisi yeyote katika utoaji wa
maamuzi mbalimbali ya kesi
Kwa upande wake afisa Tehama
wa mahakama hiyo Bw.James Kapele amesma kuwepo kwa mfumo wa kieletroniki katika
undeshaji wa kesi mbalimbali kumepunguza mlundikano wa kesi ambao ulikuwa
unajitokeza kabla ya mfumo huo wa kuanza kutumika hapanchini
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments