SERIKALI KUMALIZA KERO ZOTE ZA MAJI-WAZIRI MKUU-Septemba 21,2017
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la
upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo
mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Amesema
serikali kupitia kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo,
itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na
salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa
wilaya ya Chemba na Kondoa waliomsimamisha katika maeneo ya Chemba, Kalema,
Bicha na Bereko akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha kwa shughuli za kikazi.
Alisema
kwa sasa Serikali imeendelea na uchimbaji wa visima virefu, vifupi pamoja na
kuweka mtandao wa mabomba ya kusamba maji katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo
na ya wilaya hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo karibu na
makazi yao.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote
watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi
na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.
Aidha
Mh. Majaliwa ameagiza wakandarasi wamalize maeneo yaliyosalia katika REA awamu
ya pili ndipo waendelee na awamu ya tatu. Alisema Serikali imetenga sh.
trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado
havijaunganishiwa nishati hiyo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com,Ukuasa
wa Facebook P5Tanzania Limited
Comments