KIWANDA CHAKOSA CHOO,WANANCHI WAKERWA NA HARUFU MBAYA,MWENYE KIWANDA ARONGA-Septemba 21,2017
Kiwanda cha kupasulia magogo
kilichopo kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi chenye zaidi ya
wafanyakazi 20 hakina huduma ya choo.
Wakizi wa eneo hilo ambao hawakutaka
kutaja majina yao wamesema wanakabiliwa na harufu mbaya kwa muda mrefu kutokana
watu kujisaidia hovyo katika maeneo hayo hasa shughuli zinapoendelea kufanyika
katika kiwanda hicho.
Mmiliki wa kiwanda hicho ambaye amejitambulisha kwa jina moja la Bilali
amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuahidi kulipatia ufumbuzi ndani ya muda
mfupi.
Aidha
ameongeza kusema kuwa kiwanda hicho kilisimama uzalishaji kutokana na serikali
kusitisha uvunaji wa bidhaa za misitu hivyo kuathiri shughuli za uendelezaji wa
kiwanda hicho
Serikali kupitia mmalaka zake imekuwa ikisisitiza ujenzi wa vyoo bora katika maeneo ya makazi na taasisi mbalimbali ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com,Ukurasa
wa Facebook-P5Tanzania LimtedSerikali kupitia mmalaka zake imekuwa ikisisitiza ujenzi wa vyoo bora katika maeneo ya makazi na taasisi mbalimbali ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.
Comments