DC AAGIZA WALIOKAIDI KUFANYA USAFI WAKAMTWE
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian
Matinga ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wafanyabiasha wa soko la Buzogwe katika
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baada ya kukaidi agizo la kufanya usafi katika
maeneo ya soko hilo.
DC Lilian Matinga Picha na Issack Gerald |
Matinga ametoa agizo hilo leo wakati
akishiriki zoezi la usafi katika soko la Buzogwe akiwa ameambatana na maafisa
wa jeshi la polisi pamoja na watumishi wakiwemo watumishi wa umma.
Amesema kuwa katika soko hilo hakuna aliyefanya
usafi zadi ya mwenyekiti wa soko ambapo amesema watakaochukuliwa hatua watawajibishwa
kwa kulipa faini ya shilingi 50,000 ikiwezekana hata kupelekwa mahabusu.
Baadhi ya wananchi ambao wameshiriki zoezi la usafi
wamesema kama serikali itaendelea kuhamasisha usafi mara kwa mara hakutakuwa na
hofu ya magonjwa ya mlipuko.
Jana mkuu wa mkoa wa Katavi Meja
Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,aliagiza watumishi wa umma na wananchi
kushiriki katika zoezi la usafi kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka
46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani
Karume aliyefariki dunia Aprili 7 mwaka 1972 kwa kupigwa risasi hadharani
wakati akicheza bao.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments