KATAVI WAFANYA USAFI WAADHIMISHA KIFO CHA KARUME
Serikali ya Mkoa wa Katavi umefanya
zoezi la usafi kama sehemu ya kuadhimisha miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza
wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani
Karume.
Katika taarifa iliyokuwa imetolewa
jana na Afisa Habari wa Manispaa ya Mpanda Pius Donald alikuwa amebainisha
maeneo yanayofanyiwa usafi kuwa ni pamoja na maeneo ya hospitali,sokoni na
stendi kuu.
Serikali imekuwa ikiwataka watanzania
kufanya usafi wa hali ya juu katika maeneo yao ili kuendelea kuwa salama
ikiwemo kuepuka maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindipindu ambapo imekuwa
ikifikia hatua ya kuchukua hatua kali za kisheria wa watu wanaokaidi kufanya
usafi katika maeneo yao.
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
alizaliwa mwaka 1905 na alifariki dunia tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi
hadaharani wakati akicheza bao huko Zanzibar.
Habari zaidio ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments