WANANCHI MKOANI KATAVI WAASWA KUMUENZI NYERERE KWA KUDUMISHA AMANI
Ikiwa kesho ni kilele cha mbio za
mwenye wa uhuru na kumbukumbu ya kifo cha Hayati Julius Nyerere,wakazi Mkoani Katavi
wamesema kumbukumbu ya miaka 18 tangu kifo cha hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere inafaa kutumika
kuyaenzi kwa kudumisha amani na mshikamano .
Kwa nyakati tofauti wamesema uzalendo
wa Baba wa Taifa umeliunganisha taifa na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa
utambulisho wa Mtanzania.
Aidha wameongeza kusema kuwa
viongozi wa sasa wanapaswa kueendelea kudumisha demokrasia ikiwemo kuheshimu
katiba ili kuendeleza dhana ya utawala bora ambayo muasisi wake ni hayati Mwalim
Julius Kambarage Nyerere.
Zoezi la kuuzima mwenge wa Uhuru
visiwani Zanzibar litafanyika kesho katika viwanja vya
amani huku likiwa sambamba na kumuenzi baba wa Taifa Mwl.julius Kambarage
Nyerere ambapo kumbu kumbu hiyo hufanyika kila ifikapo tarehe 14mwezi October.
Comments