KILELE WIKI YA VIJANA,VIJANA MKOANI KATAVI WASHAURIWA KUJIAJIRI
BAADHI ya vijana katika Manispaa ya
Mpanda Mkoani Katavi,wamewashauri vijana wenzao kufanya kazi kwa bidii kama
sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana hapa nchini.
Vijana hao wakiwemo Goodluck Valanti
na Ngosha Doni wamesema kuendelea kusubiri kuajiliwa hakutawasaidia kuondokana
na umaskini na badala yake vijana wajitambue kwa kufanya kazi kwa malengo.
Kilele cha wiki ya vijana hutoa
nafasi kwa jamii na serikali kujadili masuala ya vijana ilikwemo masuala ya
kiuchumi ambapo serikali imekuwa ikihamasisha vijana kujiunga katika vikundi
vya ujasiliamali ili wawezeshwe kujikwamua kiuchumi.
Wiki ya vijana hapa nchini
hadhimishwa sambamba na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru pamoja na kumbuku ya
kifo cha Hayati Julius Nyerere kila ifikapo Oktoba 14 kila mwaka ambapo
kaulimbiyu mwaka huu inasema ‘’Shiriki
kukuza uchumi wa viwanda kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu’’.
Comments