RAIS MAGUFULI AWASILI ZANZIBAR KUJIANDAA KUZIMAMWENGE WA UHURU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli,amewasili Zanzibar kwa ajili kuhitimisha kilele cha mbio za mwenge wa uhuru hapo kesho.
Rais Dkt John Maguli akishuka katika uwanja wa ndege wa Amani
Rais Magufuli mara baada ya kuwasili visiwani Zanzibar amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Grayson Msigwa amesema Rais Magufuli atakuwepo visiwani Zanzibar kwa siku tatu.
Pamoja na kuhitimisha kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu,pia Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha siku ya Mwalimu Nyerere.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA